WAJUMBE kutoka nchini za za Kiarabu katika Umoja wa Mataifa wameunga mkono pendekezo la Palastina kuhimiza makubaliano ya Amani pamoja na Israel mnamo muda wa mwaka mmoja unaokuja na kumaliza kukaliwa ardhi za Wapalastina na Israel hadi ifikapo mwaka 2017, licha ya upinzani wa Israel na Marekani.
Taarifa zaidi zimeeleza kuwa bado haijafahamika ni lini haswa mswaada wa azimio hilo utapigiwa kura katika Baraza la Usalama.