NAIBU Waziri wa Maendelea ya Jamii,Jinsia na Watoto Dokta PINDI CHANA ameitaka Jamii kutunza Mazingira ili kulinda Afya ya Mtoto.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Dokta PINDI ameeleza kuwa mtoto anatakiwa kupata haki za Msingi ikiwemo ya kulindwa,kutunzwa,kuendelezwa,kuishi,kushirikishwa pamoja na kutobaguliwa.
Amebainisha kuwa Ulinzi wa Mtoto unahitajika dhidi ya Ukatili kwa kutoa taarifa kwenye vyombo vya Sheria ili kumsaidia kupata mahitaji muhimu ikiwa ni pamoja na Mavazi,Malazi na Chakula.