MAMA WAJAWAZITO Wilayani Kahama Shinyanga wameaswa kuacha tabia ya kujifungulia nyumbani na kutumia dawa za kienyeji wakati wa kujifungua.
Badala yake wamehimizwa kujifungulia hospitali ili kupata msaada wa Madaktari kuhakikisha Usalama wao.
Ushauri huo umetolewa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kahama Dokta JOSEPH NGOWI wakati wa uzinduzi wa filamu iitwayo FESTULA inayoelezea athari za ugonjwa huo.