POLISI WA UWANJA wa Ndege wa Kimataifa wa Julias Nyerere-JNIA wamefanikiwa kumkamata Raia wa Kuwait,HASSAIN AHMED ALLY kwa tuhuma za kukutwa na Viumbe aina ya Kenge 149 wenye thamani ya Shilingi Milioni 6 nukta kinyume cha sheria .
Kamanda wa Polisi wa Uwanjani hapo HAMISI SELEMAN amesema kuwan raia huyo amekamatwa na Kenge hao ambao amewaweka katika mifuko midogo midogo iliyokuwa kwenye begi lake kubwa.
Amesema kuwa tukio hilo limetokea wakati HASSAN akijiandaa na safari ya kuelekea nchini Kuwait kupitia Dubai na Shirika la Emirates ingawa kati ya Kenge hao 15 walikufa huku hai wakiwa 134 .