Njia kuu ya reli inayoiunganisha Zambia na Tanzania imefungwa, baada ya wafanyakazi wake kugoma wakidai malimbikizo ya mishahara ya miezi mitano ya nyuma.
Kampuni inayosimamia njia TAZARA, ambayo anamilikiwa na Serikali ya Tanzania na Zambia, na imekuwa ikikabiliwa na uhaba wa fedha kwa zaidi ya Muongo mmoja, treni zote zimesimamishwa kwa muda usiojulikana kuanzia January 12 mwaka huu.