WAVUVI mkoani Kigoma wametakiwa kuacha tabia ya kuvua Samaki na Dagaa kwa kutumia zana haramu.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Maendeleo ya Uvuvi na Mifugo Dokta TITUS KAMANI wakati wa ziara yake ya kutembelea Mialo ya kuhifadhia Samaki na Dagaa iliyopo Kibilizi Wilayani Uvinza mkoani Kigoma.
Kwa mujibu wa Dr. Kamani, wavuvi wengi wanatabia ya kuvua samaki kwa kutumia taa zenye mwanga mkali nakusababisha samaki wengi kupofuka macho na kufa.