WANANCHI wameombwa kusaidiana na Jeshi la Polisi kutoa taarifa haraka pindi wanapoona tukio la uhalifu au kuona umiliki wa silaha kinyume na sheria ili kuweza kulinda amani na ulinzi wa Taifa .
Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Wilaya ya Temeke SOPHIA MJEMA kwenye sherehe ya utoaji sifa na zawadi kwa Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali.
MJEMA amefafanua kuwa ni muhimu wananchi kushirikiana na Polisi ili kuweza kupunguza matukio ya uhalifu na kuongeza usalama kwa Taifa.