VIJANA nchini wametakiwa kuachana na tabia ya kukaa vijiweni bila ya kujishughulisha na kazi yoyote, badala yake watumie fursa zilizopo za ujasirimali ili kujiajiri wao wenyewe na kupambana vilivyo na janga la umasikini.
Wito huo umetolewa na Ofisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kibaha, Leah Lwanji kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Hajat Halima Kihemba, wakati wa mkutano maalumu wa uchaguzi mkuu wa Chama cha Madereva na Wamiliki wa Pikipiki Kibaha – Chamawapiki.
Lwanji amesema kuwa nia na madhumuni ya serikali ni kuhakikisha inawakomboa vijana kuwawezesha kiuchumi ili waweze kupata ajira ambayo itawasaidia kujikimu kimaisha na kuleta chachu ya maendeleo kwa Taifa.