RAIS Barack Obama amesema harakati za kupambana na magaidi wa dola la Kiislamu zitahitaji muda, lakini zitafanikiwa.
Obama ameahidi hayo katika hotuba, juu ya hali ya nchi inayotolewa na Rais kila mwaka nchini Marekani ambapo katika hotuba hiyo, Rais Obama amelitaka Bunge la nchi yake lipitishe azimio la kuiruhusu Marekani itumie nguvu za kijeshi dhidi ya dola la kiislamu.
Rais huyo ameeleza kuwa uongozi wa Marekani katika harakati za kupambana na dola la kiislamu umewazuia wapiganaji wa kundi hilo kusonga mbele.