KUMETOKEA vurugu leo wakati wa zoezi la kuwaapisha Wenyeviti watatu wa Serikali za mitaa katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam.
Chanzo cha vurugu hizo ni baada ya Kaimu Afisa Uchaguzi Manispaa ya Ilala Hilary Baina, kumteua Bwana Mariano Haruna kuwa ni mmoja wa wagombea ambaye amepata nafasi ya Uenyekiti eneo la Kigogo Fresh B kata ya Pugu.
Kwa upande wake mgombea huyo wa Kigogo Fresh B, ambaye fanyiwa vurugu hizo, amekiri kuwa anastahiri na nimwenyekiti halali kutokana na kufata sheria, misingi na kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.