MAREKANI na Cuba zimeanza mazungumzo ya kihistoria leo kuhusu kurejesha mahusiano ya kidiplomasia baada ya kikao kilichojadili masuala ya uhamiaji kudhihirisha changamoto zilizopo katika kuondokana na uhasama wa nusu karne kati ya nchi hizo.
Ujumbe wa ngazi ya juu wa Marekani kuwahi kwenda Cuba katika kipindi cha miaka 35 utakamilisha mazungumzo ya siku mbili leo mjini Havana, huku pande zote mbili zikionya hakuna uwezekano wa kufikia makubaliano ya haraka.
Maafisa wa Marekani wanasema wana matumaini Cuba itakubali kuzifungua balozi zake na kuwateua mabalozi katika miji mikuu Washington na Havana katika miezi ijayo.