CHANJO ya majaribio dhidi ya ugonjwa wa Ebola iko njiani kuelekea nchini Liberia. Hii ni mara ya kwanza kwa chanjo hii kupelekwa kwenye nchi iliyoathiriwa zaidi na Ebola.
Lakini Wataalamu wanasema, wakati huu maambukizi ya Ebola yakiwa yanapungua, itakuwa vigumu kubaini kama chanjo hii inatoa kinga dhidi ya Virusi vya ugonjwa huo.
Chanjo hiyo ilitengenezwa na Kampuni moja ya Uingereza, na Taasisi ya kitaifa ya afya nchini Marekani GSK imesema ndege iliyo iliyobeba dozi za awali takriban 300 za chanjo inatarajiwa kufika Monrovia leo, Ijumaa.