IKULU ya Marekani imearifu kwamba rais Barack Obama na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wamezungumzia wasiwasi wao juu ya hatua ya kuongezeka mapigano mashariki ya Ukraine.
Mazungumzo ya viongozi hao kwa njia ya simu yamefanyika jana wakati rais Obama alipokuwa anarejea nyumbani baada ya kumaliza ziara yake nchini India na Saudi Arabia.
Ikulu ya Marekani imesema Obama na Merkel wamekubaliana juu ya haja ya kuibebesha dhamana Urusi kwa kuwaunga mkono waasi wanaopigania kujitenga pamoja na kushindwa kutekeleza ahadi zake chini ya makubaliano ya amani.