SERIKALI inatarajia kuweka sera ya aina moja inayounganisha sera zote nchini zinazomuhusu mtoto ijulikanayo kama Sera ya malezi, maendeleo na makuzi ya mtoto.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa utafiti wa elimu ya awali kwa watoto uliofanywa na chuo kikuu cha Aga Khan, Kaimu Mkurugenzi wa maendeleo na malezi ya watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto BENEDICT MISSANA amesema kuwa mpaka sasa serikali imeshafungua vyuo 6 vya kufundishia elimu ya awali katika maeneo mbalimbali nchini.
Amesema Vyuo hivyo vinatoa elimu maalum kwa walimu watakao fundisha shule za awali kwa lengo la kupata msingi bora wa elimu tkuanzia ngazi ya chini mpaka ngazi za juu.