UMOJA WA MATAIFA umesema mazungumzo yanayolenga kuutatua mzozo wa kisiasa nchini Yemen yanatarajiwa kurejea leo na yatasimamiwa na mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Jamal Benomar.
Taarifa kutoka umoja huo imesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amepokea vyema tangazo kuwa mshauri wake maalum kuhusu Yemen Benomar atayasimamia mazungumzo hayo na kuzitaka pande zinazopigana nchini humo kurejea katika meza ya mazungumzo kwa nia njema na kuwa na nia ya kuafikiana.
Yemen imekumbwa na mzozo tangu Rais Abed Rabbo Mansour Hadi na Waziri Mkuu kujiuzulu na waasi wa Houthi kudhibiti madaraka.