RAIS Barack Obama wa Marekani amesema atasubiri matokeo ya mazungumzo ya ngazi ya juu kuhusu Ukraine kabla ya kuamua kama Marekani itume silaha kwa serikali ya Ukraine.
Wakati akisema anapendelea diplomasia, Obama aliweka wazi suala la kuipa silaha serikali mjini Kiev.
Rais huyo wa Marekani ameyasema hayo katika mazungumzo yake na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel jana mjini Washington.