WAZIRI wa Nishati na Madini,mheshimiwa GEORGE SIMBACHAWENE amefanya ziara mkoani Lindi na Mtwara mwanzoni mwa wiki kukagua miradi mbalimbali iliyo chini ya Wizara yake ambapo ameahidi huduma za umeme na Maji kwa wananchi mbalimbali.
Akiwa Madimba mkoani Mtwara, baada ya kupokea taarifa ya Maendeleo ya Ujenzi wa Mtambo wa kuchakata gesi, Waziri SIMBACHAWENE amemwagiza Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi KAPUULYA MUSOMBA kutoa huduma ya Maji Safi kwa Wananchi wanaozunguka maeneo hayo.