MTU mmoja Mkazi wa Dar e salaam, ambaye hujishughulisha na uokotaji wa makopo ya plastiki amenusurika kifo kutokana na kipigo cha wananchi baada ya kuvunja vioo vya nyuma vya magari mawili ya wafanyakazi wa bima ya AAR yaliyokuwa yameegeshwa nje ya ofisi hizo.
Kijana huyo aliyekuwa na jeraha upande wa nyuma wa kichwa chake kikivuja Damu nyingi amejitambulisha kwa jina Amir Ismail na kuiambia EFM kuwa kuna vijana sita wamemvamia na kumpora fedha zake shilingi elf 60 alizokuwa nazo.
Ismail ameeleza kuwa baada ya kuporwa pesa zake ndipo aliamua kuokota mawe na kupiga vioo vya magari hayo, kitendo kilichowakasirisha watu hao na kuanza kumpiga.