ESCROW: CHENGE APANDISHWA KIZIMBANI

ESCROW: CHENGE APANDISHWA KIZIMBANI

Like
331
0
Wednesday, 25 February 2015
Local News

MBUNGE wa Bariadi Magharibi kupitia chama cha Mapinduzi -CCM, Andrew Chenge amepandishwa kizimbani  kwa madai ya kukiuka maadili ya viongozi wa umma, chini ya Tume  ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Baraza la Maadili lililoketi,  jijini Dar es Saalam asubuhi ya leo.

Katika shauri linalomkabili Chenge ni dhidi ya kukiuka vifungu hivyo vya sheria ya maadili ya viongozi wa umma, ambapo ilielezwa kuwa, Miongoni mwa makosa anayokabiliwa nayo ni pamoja na alipokuwa  Mtumishi  mkuu wa serikali kwa  wadhifa wa mwanasheria Mkuu wa Serikali AG,  alipitisha mikataba mbaalimbali dhidi ya  IPTL, na baadae alipostaafu nafasi hiyo ya Mwanasheria Mkuu  alikuwa miongoni mwa Washauri wakuu wa kampuni ya V.I.P Engineer.

Imeelezwa kuwa, Chenge hakuwahi kueleza tume hiyo ya Maadili kama ana madai ama ana hisa na kampuni hiyo ya V.I.P ambayo iliingia ubia na IPTL Katika uuzwaji wa hisa hali ambayo moja kwa moja ilipelekea kukiuka vifungu vya sheria.

Comments are closed.