Matumaini ya Arsenal kufikia robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya kwanza toka mwaka 2010 yanakutana na vikwazo mara baada kupokea kichapo cha 3-1 kutoka kwa Monaco katika uwanja wao wa nyumbani huko Emirates
Meneja wa timu ya Arsenal ametupia lawama kwa wachezaji wake kwa kusema kuwa kiakili hawakuwa wamejiandaa kwenye mchezo huo baada ya kuruhusu magoli yaguse mlango wao kutoka kwa Geoffrey Kondogbia, Dimitar Berbatov na Yannick Ferreira
Alex Oxlade aliipatia bao Arsenal lililodumu hadi mwisho wa mchezo, kwa matokeo ya mchezo huo yanaiweka Arsenal kwenye hali ngumu kwenye mechi ya marudiano wanahitajika angalau kushinda magoli matatu katika uwanja wa nyumbani wa Monaco hapo march 17
Beki wa Arsenal Per Mertesacker akionekana kusikitishwa na goli la kwanza waliofungwa na klabu ya AS Monaco usiku wa jana katika mechi ya klabu bingwa Ulaya. Arsenal waliruhusu kichapo cha magoli 3-1 katika uwanja wa nyumbani.
Mshambuliaji wa klabu ya AS Monaco, Dimitar Berbatov akishangilia goli baada ya kuifunga klabu ya Arsenal katika ushindi wa magoli 3-1 ndani ya uwanja wa Emirates.