KATIBU MKUU wa NATO Jens Stoltenberg ameonya kwamba jaribio lolote la kupanua mipaka inayoshikiliwa na wapiganaji wanaotaka kujitenga nchini Ukraine , halitakubalika na kuiambia Urusi kuondoa vifaa 1,000 vya kijeshi kutoka katika ardhi ya nchi jirani ya Ukraine.
Akizungumza baada ya mkutano na waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi , katibu mkuu wa NATO ameeleza matumaini ya tahadhari juu ya matarajio ya makubaliano tete ya kusitisha mapigano kati ya waasi wanaoungwa mkono na Urusi na majeshi ya Ukraine.
Matamshi ya Stoltenburg yanakuja wakati jeshi la Ukraine limetangaza kuanza kuondoa silaha kali kutoka katika mstari wa mbele wa mapambano.