MAKAMU wa Rais wa Sierra Leone SAMUEL SAM-SUMANA amejiweka mwenyewe katika Karantini kwa siku 21 baada ya mlinzi wake mmoja kufa Jumanne iliyopita kutokana na ugonjwa hatari wa Ebola. SAM-SUMANA anakaimu wadhifa wa Urais baada ya rais Wa nchi hiyo ERNEST KOROMA kuondoka Sierra Leone kwenda Ubelgiji kuhudhuria mkutano kuhusu Ebola utakaofanyika March. SAM-SUMANA anatekeleza majukumu yake kutoka nyumbani kwake na ni Kiongozi wa kwanza wa ngazi ya juu wa Afrika kuwa katika Karantini tangu Mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola ulipozuka Afrika Magharibi, huku idadi ya vifo Ikikaribia 1,000.