IRAQ imeanzisha operesheni kubwa ya kuukomboa mji wa Tikrit unaodhibitiwa na kundi la Dola la Kiislamu.
Wanajeshi Elfu-30 wa Iraq na wapiganaji wakisadiwa na ndege za kivita wamezishambulia ngome za wapiganaji wa jihadi wa kundi hilo ndani ya mji huo na maeneo yanaozunguka, katika harakati inayoelezwa kuwa kubwa kabisa kuwahi kufanywa kuyakomboa maeneo yanayodhibitiwa na Dola la Kiislamu.
Vikosi vya Serikali ya Iraq vimekuwa vikisonga mbele kuelekea maeneo ya Kaskazini huku vikipata ushindi dhidi ya kundi hilo lakini mji wa Tikrit umekuwa mtihani mgumu huku wapiganaji wa Dola la Kiislamu wakiwazuia wanajeshi mara kadhaa.