SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Save Vulnerable foundation linatarajia kuanzisha mradi utakao wasaidia wananchi wa Mjini na Vijijini wanaoishi katika mazingira magumu,huku waliwalenga Zaidi watu wenye matatizo ya Ulemavu katika suala la Elimu
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Shirika hilo LEONTINE RWECHUNGURA amesema kuwa ripoti ya haki za Binadamu ya mwaka 2010 na Ripoti ya Tanzania ya mwaka 2008 imethibitisha kuwa kiwango cha sasa cha Ujinga kwa watu wenye Ulemavu nchini ni Asilimia 47 nukta 6 ikilinganishwa na Asilimia 25 nukta 3, ambao hawana Ulemavu ambayo imeonyesha nusu ya watu wenye Ulemavu nchini hawapati Elimu kama inavyo stahili.
RWECHUNGURA amebainisha kuwa mradi huo utaanza katika shule za Msingi na Sekondari ambazo ni Jangwani, Pugu, na Benjamini Mkapa ikiwemo shule ya Uhuru Mchanganyiko.