BALOZI SEIF ALI IDD ALIA NA VIONGOZI WANAOKWAMISHA KURA YA MAONI KUWA NI KINYUME NA DEMOKRASIA

BALOZI SEIF ALI IDD ALIA NA VIONGOZI WANAOKWAMISHA KURA YA MAONI KUWA NI KINYUME NA DEMOKRASIA

Like
284
0
Monday, 09 March 2015
Local News

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi SEIF ALI IDD, amesema  Viongozi wa kisiasa wanaowakataza wananchi wasishiriki zoezi la kura ya maoni mwezi Aprili mwaka huu ili kuipitisha Katiba inayopendekezwa, wana alama za Udikteta na pia wanakwenda kinyume na matakwa ya Demokrasia.

Balozi SEIF ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja na kusema jambo hilo ni fedheha katika dunia mpya inayooongozwa kwa kufuata misingi ya Demokrasia na utawala bora.

Ameeleza kwamba si haki wala wajibu wa kiongozi kutoa matamshi ya kumzuia mtu au wanachama kuhusu kupiga kura na kusema jambo hilo linathibitisha wanaofanya hivyo hawako tayari kuheshimu Demokrasia.

Comments are closed.