Ronaldo avunja rekodi ya magoli kwenye ligi ya mabingwa ambapo mshambuliaji huyo alishinda mabao mawili kwenye mechi ya jana na kufikisha idadi ya magoli 78.
Klabu ya real Madrid hapo jana ilipokea kichapo cha mabao 4-3 kutoka kwa Schalke kwenye uwanja wa nyumbani.
Aidha Cristiano Ronaldo ambae ni mchezaji wa kimataifa kutoka Ureno ameapa kutozungumza chochote kwenye hadhara hadi mwisho wa msimu wa ligi hiyo
10 BORA WANAOONGOZA IDADI YA MAGOLI BARANI ULAYA PAMOJA NA UEFA SUPER CUP
78: Cristiano Ronaldo (Sporting Lisbon, Manchester United, Real Madrid)
77: Raul (Real Madrid, Schalke)
76: Lionel Messi (Barcelona)
70: Filippo Inzaghi (Parma, Juventus, AC Milan)
67: Andriy Shevchenko (Dynamo Kyiv, AC Milan, Chelsea)
62: Gerd Muller (Bayern Munich)
62: Ruud van Nistelrooy (Heerenveen, PSV Eindhoven, Manchester United, Real Madrid, Hamburger)
59: Thierry Henry (Monaco, Arsenal, Barcelona)
59: Henrik Larsson (Feyenoord, Celtic, Barcelona, Helsingborgs)
56: Eusebio (Benfica)
Richa ya matokeo hayo ya jana Real Madrid imepita kwenye hatua ya tano katika robo fainali za ligi ya mabingwa