WIZARA ya maji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni imefanya Operesheni ya kukamata wezi wanaoiba Miundo mbinu ya maji ili kuondoa kero ya upatikanaji wa maji katika sehemu mbalimbali jijini dar es salaam.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini dar es salaam Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, PAUL MAKONDA amesema kuwa, katika oparesheni hiyoWilaya ya Kinondoni ni mojawapo ya wilaya ya Mkoa wa Dar es salaam zilizohujumiwa na kuwa na wizi mkubwa wa maji katika miundo mbinu yake.
Aidha amesema kuwa gharama za maji zinapanda kutokana na watu wachache wanaoiba maji hivyo amewataka wananchi kutowafumbia macho wahalifu hao kwani kwa kufanya hivyo bei ya huduma za maji itashuka tofauti na ilivyo sasa.