WAKATI Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia kuanza Machi 17 mwaka,Taasisi za ukusanyaji fedha nchini zikiwemo Halmashauri zimetakiwa kutekeleza wajibu wake, ili kuwezesha lengo la Bajeti kufikiwa badala ya kutegemea fedha kutoka Hazina pekee.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha MWIGULU NCHEMBA wakati akizungumza na EFM kuhusu changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa Bajeti, ambapo amesema Halmashauri zikiwajibika ipasavyo kukusanya fedha na Wizara zenye wajibu wa kukusanya Maduhuli zikitekeleza kazi hiyo zitasaidia katika utekelezaji wa Bajeti.
NCHEMBA amesema pamoja na kazi inayofanywa na Mamlaka ya Mapato nchini -TRA kusaidia katika ukusanyaji wa fedha, bado Serikali inahitaji kuvitumia vyanzo vingine vya mapato ili kuhakikisha lengo linalokusudiwa na Bajeti linafikiwa kwa wakati.