MKUU wa Mkoa wa Katavi Dokta IBRAHIMU MSENGI ameagiza Wanafunzi waliohitimu Elimu ya Msingi mwaka 2014 na kufaulu kwa kuchaguliwa kujiunga na Elimu ya Sekondari, waripoti katika shule walizopangiwa.
Dokta MSENGI ametoa kauli hiyo katika Hotuba yake iliyosomwa kwa Niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Mstaafu ISSA SELEMAN NJIKU, wakati akifungua kikao kazi cha Viongozi,Wataalamu wa Elimu Mkoani Katavi.
Mkuu huyo wa Mkoa amehimiza kukomeshwa kwa Watoro Mashuleni Wanafunzi walioacha shule wasakwe, na kurudishwa shuleni ili waendelee na masomo.