WANANCHI wa Nigeria kesho wanatarajiwa kujitokeza katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.
Hata hivyo kumekuwa na vuta ni kuvute huku kukiwa na Taarifa ya Mtendaji Mkuu wa Kampuni inayosambaza mashine za kusoma vitambulisho vya elekroniki vya wapiga kura kukamatwa na maafisa usalama wa nchi hiyo.
Chama kinachotawala nchini humo cha PDP kimesema kwamba mtendaji huyo Musa Sani anahusishwa na chama kikuu cha upinzani nchini humo cha APC ambaye anadhaniwa kutaka kuvuruga uchaguzi huo.