BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA LIMEPITISHA AZIMIO KUVIONGEZEA MUDA VIKOSI VYA USALAMA DRC

BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA LIMEPITISHA AZIMIO KUVIONGEZEA MUDA VIKOSI VYA USALAMA DRC

Like
273
0
Friday, 27 March 2015
Global News
BARAZA la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kuviongezea muda wa mwaka mmoja wa ziada vikosi vya kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO.
Hata hivyo idadi ya vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itapunguzwa kwa kiwango cha asilimia 10 sawa na wanajeshi 2,000.
Zaidi ya makundi thelathi ya watu wenye silaha bado yanaendelea kuhatarisha usalama wa raia hususan mashariki mwa nchi hiyo pamoja na hali ya sintofahamu ambayo imekua ikiripotiwa mara kwa mara katika mkoa wa Katanga.

Comments are closed.