MAZUNGUMZO kuhusu mpango tata wa Iran wa Nyuklia yameendelea nchini Uswisi, kwa kuwasili Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka Mataifa Sita yenye nguvu duniani.
Kiongozi wa mazungumzo wa Iran ABBAS ARAQCHI amesema makubaliano yanawezekana lakini mazungumzo yako katika hatua ngumu na bado kuna mambo ya kutatua.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza PHILIP HAMMOND pia amesema anaamini makubaliano yatafikiwa lakini yatatakiwa kuhakikisha Iran haipati uwezo wa kutengeneza bomu la nyuklia.