TETEMEKO KUBWA LA ARDHI LARIPOTIWA KATIKA PWANI YA PAPUA NEW GUINEA

TETEMEKO KUBWA LA ARDHI LARIPOTIWA KATIKA PWANI YA PAPUA NEW GUINEA

Like
240
0
Monday, 30 March 2015
Global News

TETEMEKO la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha Richter 7.6 limeripotiwa kwenye pwani ya Papua New Guinea.

Tetemeko hilo limetokea asubuhi ya leo katika eneo hilo la Asia Pasifiki.

Kituo cha Pasifiki cha tahadhari kuhusu tetemeko na Tunami lilikuwa limeonya juu ya uwezekano wa kutokea mawimbi yenye hatari katika masafa ya kilomita 1,000 kutoka kitovu cha tetemeko hilo.

Ingawa hakuna uharibifu uliotarajiwa kutokana na tetemeko hilo, nchi za eneo zima zikiwemo Papua New Guinea, visiwa vya Solomon, New Zealand, Mashariki ya Australia, Japan na visiwa vingi vya eneo hilo, zilitakiwa kuwa katika hali ya tahadhari.

Comments are closed.