KUELEKEA Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, imeelezwa kuwa Chama cha Wananchi CUF kinachounda Umoja wa Katiba wa wananchi –UKAWA, kinatarajia kumsimamisha MBARARA MAHARAGANDE kuwa Mgombea wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Morogoro mjini.
Akizungumza na Kituo hiki MAHARAGANDE amesema kuwa anauhakika wa kushinda nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu kwa kile alichodai kuwa wananchi wa Morogoro wamepania kufanya mabadiliko.
Amesema kuwa wananchi wamechoshwa na ahadi zisizotekelezeka huku hali ya maisha ikiwa duni na kukabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za miundo mbinu.