Mastar wakubwa duniani katika tasnia ya muziki wameunganisha nguvu pamoja na katika uzinduzi wa kampuni ya muziki ya Tidal.
Katika uzinduzi huo wa kampuni ya kwanza kubwa ya muziki duniani kumilikiwa na msanii Jay z uliofanyika siku ya jumatatu katika jiji la New York ulishuhudiwa na mastar ambao pia wametajwa kuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni hiyo
Miongoni mwa mastar hao ni Rihanna, Madonna, Beyonce, Usher, Daft Punk, Arcade Fire, Jack White na Kanye West.
Akizungumzia matarajio yake juu ya kampuni hiyo Alicia Keys amesema anamatumaini makubwa ya mapinduzi katika historia ya muziki kwakuthibitisha uwezo wa kampuni hiyo