SERIKALI YAAHIDI KUENDELEZA UJENZI WA BARABARA KUTOKA KIGOMA HADI KASURU

SERIKALI YAAHIDI KUENDELEZA UJENZI WA BARABARA KUTOKA KIGOMA HADI KASURU

Like
326
0
Wednesday, 01 April 2015
Local News

SERIKALI imeahidi kuendelea na utekelezaji madhubuti utakaowezesha kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya kutoka mkoani Kigoma hadi Kasuru kwa lengo la kuboresha miundombinu katika mkoa huo.

Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa JOHN MAGUFULI wakati akijibu swali la mbunge wa Muhambwe mheshimiwa FELIX MKOSAMALI aliyetaka kujua utekelezaji wa serikali juu ya suala hilo.

Waziri Magufuli ameahidi kuwa wizara itahakikisha inakamilisha ujenzi wa barabara hiyo.

Comments are closed.