WAZAZI WATAKIWA KUTODHARAU MIKAKATI YA SERIKALI JUU YA AFYA ZA WATOTO

WAZAZI WATAKIWA KUTODHARAU MIKAKATI YA SERIKALI JUU YA AFYA ZA WATOTO

Like
260
0
Wednesday, 01 April 2015
Local News

WAZAZI  nchini wametakiwa kuacha tabia ya kudharau mikakati mbalimbali ya serikali kuhusu afya za watoto na badala yake wawapeleke kupata chanjo na kuchunguza afya zao.

Aidha wazazi pia wametakiwa kuwapeleka watoto wenye chini ya umri wa miaka 15 katika zahanati na vituo mbalimbali vya afya kupima maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Rai hiyo imetolewa leo  jijini Dar es salaam na  Mkuu wa Kitengo cha akina mama na watoto wa zahanati ya Arafa Ugweno iliyopo Tandika jijini Dar es salaam Latifa Masasi  alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Zoezi hilo.

 

Comments are closed.