SERIKALI ZAIAGIZA NEC KUTOA RATIBA ITAKAYOONYESHA SHUGHULI ZA URATIBU JUU YA MFUMO WA BVR

SERIKALI ZAIAGIZA NEC KUTOA RATIBA ITAKAYOONYESHA SHUGHULI ZA URATIBU JUU YA MFUMO WA BVR

Like
259
0
Thursday, 02 April 2015
Local News

KATIKA kuhakikisha kuwa zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kupitia mfumo wa –BVR- linafanikiwa serikali imeiagiza tume ya Uchaguzi nchini –NEC– kuandaa ratiba itakayosaidia kuonesha shughuli zote za uratibu wa zoezi hilo.

Agizo hilo limetolewa na Waziri Mkuu Mheshimiwa MIZENGO PINDA mjini Dodoma wakati akifunga rasmi kikao cha kumi na tisa cha Bunge ambapo amesema kuwa ni muhimu kwa ratiba hiyo kutangazwa kwa wananchi kabla ya sikuu ya PASAKA.

Waziri PINDA amesema kuwa mbali na suala la ratiba, Serikali imehakikisha inachukua jitihada katika kusambaza nakala za katiba inayopendekezwa nchi nzima yakiwemo makundi maalum ya watu ambapo kila kata imepata nakala miatatu.

 

 

Comments are closed.