HALI ya Afya ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,JOSEPHAT GWAJIMA,imebadilika ghafla baada ya kushindwa kupanda ngazi katika ofisi za Kituo Kikuu cha polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam.
Askofu GWAJIMA amefika kituoni hapo akiwa ameongozana na maaskofu zaidi ya Watano.
Katika hali ya kushangaza,wakati akipanda ngazi kuelekea kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es salaam,aliweza kupanda ngazi mbili,lakini alipojaribu ya tatu alishindwa.