VIJANA nchini wametakiwa kuacha kubweteka na kusubiri kuajiriwa na badala yake wajiajili wenyewe kwa ujasiliamali pamoja na kilimo cha kisasa.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara wa kutembelea shamba lenye ukubwa wa Ekari 300 lililopo katika kijiji cha Ngarambe wilayani Mkuranga mkoani Pwani ambalo linamilikiwa na Shirikisho la Wasanii Tanzania- SHIWATA, Mwenyekiti wa Mtandao huo Casim Taalib amesema kuwa mashamba hayo ni fursa nzuri kwa vijana kujiajiri.
Taalib amesema vijana wamekuwa na dhana tofauti ya kusubiri kuajiriwa badala ya kutambua kuwa wanaweza kujiajiri katika masuala mbalimbali na wakajikomboa kiuchumi.