POLISI WATUMIA MABOMU YA MACHOZI KUTULIZA VURUGU KUFUATIA MGOMO WA MADEREVA

POLISI WATUMIA MABOMU YA MACHOZI KUTULIZA VURUGU KUFUATIA MGOMO WA MADEREVA

Like
371
0
Friday, 10 April 2015
Local News

POLISI Jijini Dar es salaam leo wamelazimika kutumia mabomu ya Machozi kufuatia vurugu zilizoibuka Katika kituo cha mabasi cha Ubungo baada ya madereva wa vyombo mbalimbali vya moto, nchi nzima leo asubuhi kugoma kusafirisha abiria ili kuishinikiza serikali kuondoa kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa ajira za uhakika pamoja na agizo la kutaka kwenda kusoma.

Awali kabla ya mgomo wa leo, Katibu wa Muungano wa vyama vya madereva Bwana Rashid Saleh, alisema baadhi ya kero zilizopelekea mgomo wa leo ni pamoja na suala la kurudia kusoma kila wanapohuisha leseni zao ambayo wanadai ni aina nyingine ya unyanyasaji kwa maelfu ya madereva nchini, ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa hawana mfumo mzuri wa ajira licha ya kutupiwa lawama kuwa wao ndio chanzo cha ongezeko la ajali.

Katibu huyo wa Muungano wa Vyama vya Madereva alitaja kero nyingine kuwa ni hatua ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kutamka hadharani kuwa vyeti walivyonavyo madereva hao sio halali na walipanga leo kukutana na Waziri wa Kazi na Ajira kwa ajili ya kuzungumzia kero hizo kwa lengo la kuepusha kutokea kwa mgomo huo.

11148464_931930580190843_8782264410053649293_n

10985250_931930610190840_9150951142247513936_n

19711_931930550190846_1453265014833126971_n

Comments are closed.