WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Frank – Walter Steinmeier amewaalika Mawaziri wenzake kutoka Urusi, Ukraine na Ufaransa mjini Berlin siku ya Jumatatu kujadili utekelezaji wa makubaliano ya amani yaliyofikiwa mjini Minsk kuhusu mashariki mwa Ukraine, nchini Belarus Februari mwaka huu.
Mzozo kati ya waasi wanaoungwa mkono na Urusi na Majeshi ya Serikali ya Ukraine mashariki mwa nchi hiyo umesababisha watu elfu sita kupoteza maisha.
Viongozi wa Ujerumani na Ufaransa wamesimamia upatikanaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano mjini Minsk katika juhudi za kusitisha umwagikaji wa damu , na uhasama umepungua licha ya kuwa tofauti bado zipo katika kupiga hatua.