RAIS KIKWETE AUNGANA NA WAUMINI WA KANISA KATOLIKI SHINYANGA KUMSIMIKA ASKOFU MPYA

RAIS KIKWETE AUNGANA NA WAUMINI WA KANISA KATOLIKI SHINYANGA KUMSIMIKA ASKOFU MPYA

Like
460
0
Monday, 13 April 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameungana na maelfu ya waumini wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Shinyanga, kuhudhuria Ibada rasmi ya kumweka wakfu na kumsimika Askofu mpya wa Jimbo hilo, Mhashamu Baba Askofu Liberatus Sangu.

Rais Kikwete aliwasili kwenye Kanisa Kuu la Mama Mwenye Huruma, Ngokolo, mjini Shinyanga jana  kwa ajili ya Ibada hiyo iliyohudhuriwa pia na Maaskofu wakuu, maaskofu na maaskofu wasaidizi 38, akiwamo Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na Rais wa Mabaraza ya Kipapa na Katibu Mwambata wa Uenezaji Injili Ulimwenguni Askofu Mkuu Protase Rugambwa kutoka Makao Makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican.

Askofu Sangu ambaye amewekwa wakfu na kusimikwa kwenye Siku ya Huruma ya Mungu Duniani anakuwa Askofu wa nne wa Jimbo la Shinyanga na anachukua nafasi iliyoachwa wazi tokea Novemba 6, mwaka 2012, wakati aliyekuwa Askofu wa Jimbo hilo, Baba Askofu Aloysius Balina alipofariki dunia.

unnamed (12)

unnamed (13)

 

Comments are closed.