UCHAGUZI Mkuu nchini Sudan umeanza leo huku dalili zikionesha kwamba Rais wa sasa wa nchi hiyo OMAR AL BASHIR anatarajiwa kushinda kiti hicho cha Urais.
Taarifa zinasema kuwa Vyama vingi vya upinzani vimesusia uchaguzi huo kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ukandamizaji wa kisiasa unaoendeshwa na rais OMAR AL BASHIR.
Hata hivyo inaaminika kuwa Rais BASHIR alifanya kampeni kubwa akihutubia mikutano ya hadhara sehemu tofauti za taifa hilo kubwa na kwamba ndiye kiongozi pekee wa nchi aliyewekewa hati ya kukamatwa na Mahakama ya kimataifa ya ICC.