Wanachama kumi wa shirikisho la soka la Amerika ya kaskazini, America ya kati na muungano wa visiwa vya Caribbea (Concacaf) kwa pamoja wamefikia maamuzi ya kumuunga mkono Rais wa shirikisho la soka duniani Sepp Blatter katika uchaguzi wa FIFA hapo May.
Azimio hilo la kumuunga mkono Blatter limefanywa katika mkutano wa (Concacaf). Rais wa chama cha soka cha jamhuri ya Dominic Osiris Guzman, amemfananisha rais huyo wa FIFA na watu mashuhuri walioweka historia duniani ikiwemo Moses, Abraham Lincoln na Martin Luther King.
“Jumuia inatuma ujumbe kuwa “tunaendelea kumuunga mkono Blatter” alisema rais wa Concafaf Jeffrey Webb.Blatter ambaye ni raia wa Uswiss ni mmoja kati ya wagombea wa nne. Wengine ni pamoja na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ureno Luis Figo, Mholanzi Michael van Praag, na mwana mfalme Prince Ali Bin Al Hussein ambaye alikuwa pamoja na Blatter katika mkutano huo wa Alhamis japokuwa akuhutubia.