JAMII imeombwa kutodharau Elimu na kuipa kipa umbele kwa kuhakikisha kuwa watoto wanasoma kwa bidii ili na kutimiza ndoto zao za maisha kwakuwa maendeleo na mabadiliko ya Taifa yanategemea sana elimu na uwepo wa watoto wenye afya ya mwili na akili.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Muungano wa vijana wa maendeleo na ushirikiano Tanzania-TAYDCO katika kampeni maalum ya Malaria ya kusaidia watoto wasiojiweza kama walemavu na yatima.
Akizungumza na Efm, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Aloyce Masana amesema adui wa kwanza wa maendeleo ni kukata tamaa hivyo amewataka watoto kuwa wabunifu kupitia elimu.