SERIKALI imeombwa kuongeza wataalamu wa kupanga madaraja ya Tumbaku ili kuwawezesha wakulima kupata bei nzuri kwenye soko la zao hilo.
Pia imeombwa kutafuta wawekezaji wengine na masoko nchini China,baadala ya kutegemea kampuni tatu zinazonunua Tumbaku mkoani Tabora,jambo ambalo litawasaidia wakulima kupata soko la uhakika.
Ombi hilo imetolewa na Mbunge wa Viti maalumMkoa wa Tabora,MAGRETH SITTA,alipokuwa akichangia makadirio ya Ofisi ya Waziri Mkuu,ambapo amesema zao hiloni muhimu kwa kuwa linaiingizia serikali asilimia 50 ya mapatoya fedha za kigeni.