MAMLAKA ya udhibiti na manunuzi ya Umma nchini PPRA imesema kuwa ndani ya kipindi cha miaka 10 imebaini kuwa katika ofisi nyingi za Umma kumekuwepo ubadhirifu mkubwa wa fedha kwenye masuala mbalimbali yanayohusiana na ununuzi.
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Doroth Mwanyika wakati wa ufunguzi wa semina iliyoandaliwa na PPRA yenye lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari nchini kuandika habari zinazohusu manunuzi ya umma.
Amebainisha kuwa katika kipindi ambacho taasisi hiyo imeanzishwa mpaka sasa wamegundua wizara nyingi pamoja na Halmashauri mbalimbali nchini kutawaliwa na ubadhirifu huo hususani kwenye sekta ya manunuzi