THAILAND, MALAYSIA NA INDONESIA ZAKUTANA KUJADILI TATIZO LA WAHAMIAJI HARAMU

THAILAND, MALAYSIA NA INDONESIA ZAKUTANA KUJADILI TATIZO LA WAHAMIAJI HARAMU

Like
183
0
Wednesday, 20 May 2015
Global News

MAWAZIRI wa Mambo ya Nje wa Thailand, Malaysia na Indonesia wanafanya mkutano wa dharula mjini Kuala Lumpur kujadili tatizo la wahamiaji haramu katika ukanda wao.

Nchi hizo tatu zinakabiliwa na shinikizo la kimataifa kuwasaidia maelfu ya wahamiaji waliokwama Baharini ambao wanahitaji chakula na maji.

Wahamiaji wengi ni waislamu wa jamii ya Rohingya waliokimbia Myanmar, lakini Serikali ya nchi hiyo imekataa kuhudhuria mkutano huo. Bado kuna hofu kuhusu usalama wa waliokwama baharini.

 

Comments are closed.