SERIKALI KUSHIRIKIANA NA UNESCO KUADHIMISHA WIKI YA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA UNESCO KUADHIMISHA WIKI YA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA

Like
282
0
Wednesday, 20 May 2015
Local News

SERIKALI ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni- UNESCO inatarajia kuadhimisha wiki ya Ukombozi wa Bara la Afrika Mei 25 hadi 29 mwaka huu.


Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Assah Mwambene ,amesema maadhimisho hayo yanatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe.


Katika ufunguzi huo, Mwambene ameeleza kuwa maadhimisho hayo yatatanguliwa na uzinduzi wa Mradi wa Nyaraka za Urithi wa Tanzania –TAHAP, ikiambatana na maonyesho ya picha ya kumbukumbu mbalimbali zinazoelezea ukombozi wa bara hilo.

Comments are closed.